Phiri amesema anaendelea kumuomba Mungu amjalie afya njema na amuepushe na majeraha ili mzunguko wa pili arudi kwa kasi ya kufunga zaidi.
Phiri ameongeza kufunga mabao hayo kunatokana na ushirikiano anaoupata kutoka kwa wachezaji wenzake huku akikiri anazungukwa na nyota wenye uwezo mkubwa.
"Kufunga mabao 10 kwenye mzunguko wa kwanza kumeniongezea morali, hii ni mara ya kwanza kucheza Ligi ya Tanzania lakini namshukuru Mungu naendelea vizuri, kikubwa namuomba Mungu aniepushe na majeraha ili mzunguko wa pili niendelee kuisaidia timu," amesema Phiri.
Akizungumzia kucheza mechi tatu bila kufunga Phiri amesema: "wakati mwingine inakuwa ngumu na inakufanya kuwa na presha ukizingatia Simba ni timu kubwa na mashabiki wanahitaji ushindi lakini unapaswa kutuliza akili na baadae mambo hukaa sawa."