Simba Sports Club
News

Kauli ya Pablo kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Kagera

10 May 2022

Pablo amesema hatua ilipofikia ligi kila mchezo unakuwa mgumu na kila timu inahitaji pointi tatu ili kujiweka vizuri katika msimamo.

Pablo ameongeza kuwa ingawa tutakosa baadhi ya wachezaji wetu wa kikosi cha kwanza kutokana na majeruhi lakini tutahakikisha tunashinda ili kuwapa furaha mashabiki wetu.

"Mchezo utakuwa mgumu, Kagera ni timu nzuri na tunakumbuka walitufunga katika mchezo wa mzunguko wa kwanza ingawa nasi tulipoteza nafasi nyingi za kufunga.

Advertisement

"Tunahitaji kuwapa furaha mashabiki ambao mara zote wamekuwa nasi katika nyakati za furaha na huzuni. Tutawakosa baadhi ya wachezaji wetu muhimu kutokana na kuwa majeruhi lakini waliopo wapo tayari kupambana," amesema Pablo.

Akizungumzia changamoto ya kufungwa mara kadhaa kwa mipira ya kutengwa Pablo amesema wanaendelea kuifanyia kazi mazoezini na kadiri muda unavyokwenda ndivyo inavyopungua.

Back to homepage
Share this story