Pablo amesema baada ya kutoka kwenye Michuano ya Mapinduzi hatukupata muda wa kufanya mazoezi na tukaenda kucheza mechi ngumu na kujikuta tumepoteza.
Raia huyo wa Hispania ameongeza kuwa baada ya City kupata bao wachezaji wao walikuwa wanapoteza muda makusudi na kuwatoa mchezoni nyota wetu.
Advertisement
"Tulijua mchezo ungekuwa mgumu kutokana na ubora wa wapinzani, hatukupata muda wa maandalizi na pia uwanja haukuwa bora hivyo vyote vimechangia.
"Wachezaji walijitahidi kufanya kila linalowezekana kuhakikisha tunapata matokeo, ilibidi tubadili mfumo baada ya City kuwa pungufu lakini bado haikusaidia," amesema Pablo.