Simba Sports Club
News

Kauli ya Pablo baada ya droo ya makundi Shirikisho

29 Dec 2021

Kocha Mkuu Pablo Franco, amesema kundi letu katika hatua ya makundi ya Shirikisho Afrika si jepesi hivyo tutapaswa kuwa makini katika kila mchezo ili kuhakikisha tunafikia malengo tuliyojiwekea.

Pablo amesema wakati anapewa jukumu la kukinoa kikosi aliiambiwa malengo yetu ni kufika nusu fainali ya michuano hiyo, hivyo maandalizi yanapaswa kuanza mapema.

Amesema kila timu katika kundi ni ngumu na kwenye michuano hii kadri muda unavyosonga mbele ndiyo ugumu unaongezeka lakini tuko tayari kupambana kuhakikisha tunafikia malengo yetu.

Advertisement

"RS Berkane ni timu nzuri tena ina nyota wetu wa zamani Clatous Chama tunajua haitakuwa rahisi kuwakabili. Asec Mimosas ni timu kongwe Afrika na ina uzoefu mkubwa wa michuano hii.

"Gendamarie nayo si timu ya kubeza, mchezo uliopita dhidi ya Red Arrows ulikuwa mgumu kwa hiyo hatutaidharau kwa namna yoyote kila mchezo utakuwa fainali kwetu hadi tutimize malengo yetu," amesema Pablo

Back to homepage
Share this story