Meneja wa Timu Patrick Rweyemamu, amesema kikosi kiko tayari kupambania alama tatu dhidi ya KMC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC utakaopigwa Ijumaa katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi saa 10 jioni.
Rweyemamu amesema kikosi cha wachezaji 24 kilichosafiri mkoani hapa wako kwenye nzuri na wapo tayari kwa ajili ya mchezo ambao tunaamini utakuwa mgumu lakini tumejipanga kuhakikisha tunaibuka na ushindi.
Advertisement
"Kikosi kimefika salama Tabora, wachezaji wako vizuri na jioni watafanya mazoezi ya kuweka sawa miili kutokana na uchovu wa safari.
"Tumekuja na wachezaji 24 na watu 14 wa benchi la ufundi tayari kwa mchezo, tunajua mchezo utakuwa mgumu sisi ni mabingwa watetezi kwa hiyo tumejipanga kuhakikisha tunashinda," amesema Rweyemamu.