Simba Sports Club
News

Kauli ya Matola kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Petro De Luanda

22 Nov 2025

Matola amesema hatujawahi kukutana na Petro hapo kabla na tunaiheshimu kutokana na ubora walionao lakini tumejipanga na itakuwa vizuri kupata ushindi kwenye mchezo wa kwanza.

Matola ameongeza kuwa wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri tayari kwa mchezo huo huku akiwaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi ili kuwapa chachu ya kutafuta alama tatu.

"Kikosi kipo tayari kwa mchezo wa kesho, tunafahamu haitakuwa mechi rahisi Petro ni timu imara lakini tumejipanga na tupo tayari."

Advertisement

"Kuna ugumu wa kucheza na timu ambayo haujuani nayo lakini tuna uzoefu mkubwa kwenye mashindano haya na tumejipanga kufanya vizuri ili kuwapa furaha mashabiki," amesema Matola.

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji, kiungo mshambuliaji Joshua Mutale amesema wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo ingawa anaamini utakuwa mgumu.

"Tumepata maandalizi mazuri kutoka kwa walimu wetu na kwakifupi tupo tayari kwa mchezo hata kama utakuwa mgumu tunahitaji kupata ushindi nyumbani," amesema Mutale.

Back to homepage
Share this story