Matola amesema wachezaji wote tuliosafiri nao wapo kamili na tutaingia kwenye mchezo kwa lengo la kutafuta pointi tatu ugenini.
Aidha Matola ameongeza kuwa utakuwa mchezo mgumu kutokana na ubora walionao Coastal hasa ukizingatia wapo nyumbani lakini tumejiandaa vizuri kuwakabili.
"Itakuwa mechi ngumu, Coastal ni timu bora kwa sasa. Kuna mapungufu yalionekana kwenye mchezo uliopita dhidi ya Tanzania Prisons tumeyaona na tunayafanyia kazi."
Akizungumzia hali ya wachezaji Matola amesema "Henock Inonga alipata majeraha kwenye mchezo uliopita na amerejea Dar es Salaam kwa ajili ya vipimo lakini Willy Onana yeye amepona na yupo tayari kwa mchezo wa kesho."
Akiongea kwa niaba ya wachezaji mlinda mlango Ally Salim amesema "sisi kama wachezaji tupo tayari kupambana dhidi ya Coastal kesho, itakuwa mechi ngumu lakini tumejipanga lengo ni kupata pointi zote tatu."