Simba Sports Club
News

Kauli ya kocha Zoran kuelekea mchezo dhidi ya Kotoko

28 Aug 2022

Zoran amesema mchezo utakuwa kipimo kizuri na kitawapa maandalizi bora wachezaji wetu kuelekea kurejea kwa ligi pamoja na michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Zoran ameongeza kuwa wachezaji ambao hawajapata dakika nyingi za kucheza katika mechi zetu zilizopita atawapa nafasi kubwa ya kucheza ili kupata muunganiko.

Advertisement

"Itakuwa kipimo kizuri kwetu, Asante Kotoko ni timu kubwa ni mabingwa wakwao na ipo kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika itatupa mazoezi mazuri.

"Kuna wachezaji ambao hawakupata muda mwingi wa kucheza katika mechi zetu zilizopita tutawapa nafasi ili kupata michezo ya ushindani nakuwaweka sawa," amesema Zoran.

Back to homepage
Share this story