Simba Sports Club
News Videos

Kauli ya Kocha Wilken kuelekea mchezo dhidi ya Fountain Gate

5 Feb 2025

Wilken amesema mchezo utakuwa mgumu hasa kutokana na Fountain Gate kuwa nyumbani lakini tumejiandaa vizuri kuhakikisha tunapata pointi tatu muhimu ugenini.

Wilken ameongeza kuwa mzunguko wa pili wa ligi ni mgumu na kila timu imejipanga kuhakikisha inafanya vizuri hasa ikiwa nyumbani lakini tumejiandaa kupambana na changamoto yoyote itakayojitokeza.

"Maandalizi yamekamilika, kikosi kimefika leo Manyara na jioni kitafanya mazoezi ya mwisho kwa ajili ya mchezo wa kesho ambao tunaamini utakuwa mgumu," amesema Wilken.

Advertisement

Kwa upande wake nahodha wa timu Mohamed Hussein 'Zimbwe Jr' amesema kwa upande wao wachezaji wapo tayari kupambana hadi mwisho kuhakikisha alama tatu zinapatikana.

"Malengo yetu kwenye kila mchezo ni kuhakikisha tunapata alama tatu, kwetu kila mechi ni fainali na tupo tayari kupambana hadi mwisho ili kufanikisha hilo," amesema Zimbwe Jr.

Back to homepage
Share this story