Simba Sports Club
News

Kauli ya Kocha Nkoma baada ya ushindi dhidi ya Alliance

12 Jan 2022

Kocha Mkuu wa Timu ya Simba Queens, Sebastian Nkoma amekiri licha ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Alliance Girls lakini mchezo ulikuwa mgumu kutokana na kuwakosa baadhi ya nyota wetu.

Nkoma amesema katika mchezo wa leo tuliwakosa wachezaji kadhaa ambao wamejiunga na timu ya taifa huku wengine wakiwa majeruhi.

Nkoma ameongeza kuwa alilazimika kufanya mabadiliko ya kikosi kutokana na kuwakosa nyota wake hao huku akiwamwagia sifa Alliance kwa jinsi walivyocheza.

Advertisement

"Mchezo ulikuwa mgumu hasa kipindi cha kwanza. Tumewakosa baadhi ya wachezaji wetu kutokana na kuitwa timu za taifa na wengine ni majeruhi.

"Lazima niwapongeze Alliance wamecheza vizuri. Timu yao imejaa wachezaji wengi vijana na ninaamini watakuwa msaada mkubwa kwa taifa katika siku za baadaye," amesema Nkoma.

Back to homepage
Share this story