Simba Sports Club
News Videos

Kauli ya kocha Mgosi kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Yanga Princess

8 Dec 2023

Mgosi amesema timu imepata maandalizi ya kutosha kwa muda wa miezi miwili wamefanya mazoezi sasa wachezaji wapo tayari kwa mchezo huo na mingine inayofuata.

Mgosi amesema itakuwa mechi ngumu kwakuwa ni Derby na mara zote Simba na Yanga zikikutana mchezo unakuwa mgumu lakini kwa maandalizi waliyopata anaamini tutaibuka na ushindi.

"Timu iko tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho, haitakuwa mechi rahisi na haijawahi kuwa rahisi kila tunapokutana na Yanga lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda," amesema Mgosi.

Advertisement

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji mlinzi, Violeth Nicholas amesema wapo kwenye hali nzuri kupambana kwa ajili ya kuipa timu matokeo.

"Kwa upande wetu wachezaji tupo tayari kuhakikisha tunapambana hadi mwisho kupata ushindi, tunawaheshimu Yanga na tunajua itakuwa mechi ngumu lakini tupo tayari," amesema Violeth.

Back to homepage
Share this story