Lukula ambaye amekiongoza kikosi chetu katika mechi tatu za ligi amesema timu zimefanya maandalizi mazuri na kila moja inajiandaa vizuri ikikutana nasi.
Akizungumzia mchezo dhidi ya Yanga Princess, Lukula amesema ulikuwa mgumu na wenye upinzani lakini kama tungetumia vizuri nafasi tulizopata tungeondoka na alama zote tatu.
Advertisement
"Kwa kweli ligi ni ngumu, kila timu imejipanga vizuri, ushindani ni mkubwa na umeanza mwanzoni kwa hiyo tunapaswa kujipanga.
"Unajua sisi tumetoka kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika na ndiyo mabingwa watetezi kwa hiyo kila timu ikikutana nasi inapambana vilivyo," amesema Lukula.