Kocha Mkuu, Didier Gomez amesema kikosi kipo tayari kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Tanzania Prisons utakaopigwa kesho Jumatano Machi 10, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa saa moja usiku.
Kocha Gomez amesema anaiheshimu Prisons ana anafahamu kuwa ilitufunga kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza hivyo amekiandaa kikosi kuhakikisha tunapata ushindi.
Advertisement
Gomez ameongeza kuwa ushindi kwenye mchezo wa kesho utapunguza idadi ya alama kufikia mbili dhidi ya wanaongoza ligi huku bado tukiwa na michezo mitatu mkononi.
"Kikosi kipo tayari kwa mchezo wa kesho, wachezaji wamefanya mazoezi jioni ya leo wapo kwenye hali nzuri na morali ipo juu. Tunahitaji alama tatu za kesho ili kupunguza idadi ya alama na kuwapa presha wanaongoza," amesema Kocha Gomez.