Simba Sports Club
News Videos

Kauli ya Kocha Fadlu kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Al Masry

1 Apr 2025

Fadlu amesema mchezo utakuwa mgumu kutokana na ubora wa uzoefu wa wapinzani lakini tumewaandaa wachezaji vyakutosha kuhakikisha tunapata matokeo chanya.

Fadlu ameongeza kuwa licha ya Al Masry kuwa na kocha mpya lakini bado wana kikosi imara ambacho kinaweza kuleta ushindani dhidi ya timu yoyote.

"Itakuwa mechi ngumu, lakini tumejiandaa vizuri. Kikosi chetu kimepata muda mzuri wa maandalizi na tumefanya mazoezi hapa Misri kwa siku nne na tupo tayari kwa mchezo," amesema Fadlu.

Advertisement

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji mshambuliaji, Steven Mukwala amesema wapo tayari kuhakikisha wanapigania nembo ya klabu.

"Kwa upande wetu wachezaji tupo tayari kuhakikisha tunapambana kwa dakika zote 90 ili kuwapa furaha Wanasimba wote ambao tunaamini watakuwa nyuma yetu," amesema Mukwala.

Back to homepage
Share this story