Fadlu amesema wapinzani wetu Berkane ni timu imara na ina uzoefu wa kucheza fainali lakini tumepata muda wa kujiandaa na tupo tayari kwa ajili ya kupambana na lengo ni kuchukua ubingwa.
Aidha Fadlu ameweka wazi kuwa licha ya mechi kutochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa ambao tumekuwa tukiutumia vizuri na kupata ushindi lakini hata katika dimba la Amaan Zanzibar bado tuna nafasi ya kufanya vizuri kutokana na maandalizi tuliyofanya.
"Sote tunafahamu kuwa Berkane ni timu nzuri na ina uzoefu kwenye michuano hii lakini tumejipanga na tupo tayari kwa ajili ya fainali na tunahitaji kushinda taji tukiwa kwenye ardhi ya nyumbani," amesema Fadlu.
Akizungumza kwa niaba ya wachezaji mlinzi wa kulia, Shomari Kapombe amesema wapo tayari kwa ajili ya kupambana hadi mwisho kuhakikisha tunapata ubingwa.
Kapombe amesema tunafahamu tuna kazi kubwa ya kufanya ili kupindua matokeo ingawa haitakuwa rahisi ila tupo nyumbani na tutafanya kila linalowezekana ili kuwapa furaha Wanasimba wote.
"Kila mchezaji anafahamu umuhimu wa mchezo huu na tupo tayari kuwapa furaha Wanasimba kwa kutwaa ubingwa," amesema Kapombe.