Simba Sports Club
News Videos

Kauli ya Kocha Barker kuelekea mchezo wa Singida Black Stars

10 Mar 2026

Barker amesema mipango ya timu ni kuhakikisha tunacheza soka safi na hatimaye kupata alama tatu muhimu ugenini.

Akizungumzia hali ya kikosi, Barker amesema wachezaji wote 25 tuliosafiri wote wapo kwenye hali tayari kwa mchezo wa kesho tukiwa na malengo ya kupambana hadi mwisho ili kupata alama tatu.

"Tupo tayari kwa mchezo wa kesho, tunategemea kupata upinzani mkubwa kutoka kwa Singida lakini tupo tayari kupambana hadi mwisho ili kupata matokeo chanya," amesema Barker.

Advertisement

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji kiungo mkabaji, Daud Semfuko amesema nyota wote wapo tayari kufuata maelekezo watakayopewa na walimu ili kufikia malengo tuliyojiwekea.

"Sisi kwetu kila mchezo ni muhimu wa kutafuta alama tatu, tunajua tutaenda kukutana na mpizani mgumu lakini tupo tayari kuhakikisha ushindi unapatikana," amesema Semfuko.

Back to homepage
Share this story