Simba Sports Club
News

Kauli ya Kocha Barker kuelekea mchezo dhidi ya TRA United

8 Apr 2026

Barker amesema ni mchezo muhimu kwetu kupata alama tatu ili kuendelea kupigania mbio za ubingwa ingawa tunaamini haitakuwa kazi rahisi kutokana na ubora wa TRA.

Barker ameweka wazi kuwa ugumu mwingine ambao tutakutanao na kesho ni kwakuwa siku chache zilizopita tulipocheza dhidi yao tuliwafunga hivyo kesho nao watataka kulipa kikosi.

"Tupo tayari kwa mchezo wa kesho, tunajua haitakuwa mechi rahisi hasa kutokana tumetoka kucheza nao siku chache zilizopita lakini tupo tayari," amesema kocha Barker.

Advertisement

Akizungumzia kuhusu hali ya kiungo mshambuliaji, Elie Mpanzu, Barker amesema "jana amefanya mazoezi na wachezaji wenzake na yupo vizuri ila hawezi kuwa sehemu ya mchezo wa kesho labda mechi ijayo dhidi ya Dodoma Jiji mwishoni mwa juma."

Kwa upande wake mlinda mlango, Hussein Abel amesema wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri na wataingia kwenye mchezo wa kesho kwa lengo moja la kutafuta alama tatu.

"Sisi wachezaji tupo tayari, tunajua itakuwa mechi ngumu lakini tupo hapa kupambana mpaka mwisho kuhakikisha tunapata alama tatu muhimu," amesema Abel.

Back to homepage
Share this story