Simba Sports Club
News

Kauli ya Kocha Barker kuelekea mchezo dhidi ya Mashujaa

28 Jan 2026

Barker amesema wachezaji wapya wanaingia pole pole kwenye kikosi na maendeleo ya timu kwa ujumla yanaridhisha kitu ambacho kinatupa matumaini ya kupata matokeo chanya kwenye mchezo wa kesho.

Barker ameongeza kuwa amefanikiwa kutazama baadhi ya mechi za Ligi Kuu ya NBC na amebaini timu nyingi zimejiandaa na zina wachezaji wazuri ndio maana tumejipanga kuhakikisha tunafanya vizuri.

Aidha Barker ameongeza kuwa malengo ya Simba ni kupambana kwa ajili ya kupata ubingwa ndio maana kila mchezo tumeupa umuhimu mkubwa.

Advertisement

"Maendeleo ya timu yanaridhisha kila baada ya mechi tunayocheza unaona mabadiliko makubwa ya kiuchezaji hilo linatupa matumaini. Tunategemea kuwapa furaha mashabiki wetu baada ya mchezo wa kesho dhidi ya Mashujaa FC," amesema kocha Barker.

Kwa upande wake kiungo mkabaji, Daud Semfuko amesema kila mchezaji anajua umuhimu wa alama tatu katika mechi ya kesho hasa kutokana matokeo yasiyoridhisha katika michezo yetu iliyopita.

"Kwa upande wetu wachezaji tupo tayari kupambana hadi mwisho kuhakikisha ushindi unapatikana kesho, hata sisi tunaumia kwa matokeo tunayopata lakini tumejipanga kujitoa mpaka mwisho ili kuweza kuwapa furaha mashabiki," amesema Semfuko.

Back to homepage
Share this story