Barker amesema wachezaji wapo kwenye hali nzuri na morali zipo juu huku malengo yakiwa ni kuhakikisha tunashinda mchezo huo ili kutinga fainali.
Barker amekiri kuwa anafahamu utakuwa mchezo mgumu ndio maana amejiandaa kupanga kikosi chenye ushindani kulingana na ukubwa wa mechi yenyewe.
"Kikosi chetu kipo tayari kwa mchezo wa kesho, sote tunafahamu hii ni mechi kubwa na kwakuwa tunahitaji ubingwa wa michuano hii tunatakiwa kuzifunga timu zote na tumejiandaa juu hilo," amesema Barker.
Akizungumza kwa niaba ya wachezaji mlinzi wa kulia, David Kameta 'Duchu' amesema wachezaji wapo tayari kuhakikisha wanapambana mpaka mwisho ili ushindi upatikane.
Duchu ameongeza kuwa anaamini utakuwa mchezo wa tofauti hasa baada ya kupata kocha mpya kwakuwa amekuja na mbinu tofauti na kila mchezaji anataka kuonyesha uwezo wake ili apatiwe nafasi.
"Tupo tayari kwa mchezo wa kesho, kama alivyosema kocha malengo yetu ni yale yale tunautaka ubingwa wa Kombe la Mapinduzi," amesema Duchu.