Barker amesema amewafuatilia TRA katika mchezo wao uliopita dhidi ya watani na kujiridhisha kuwa ni timu imara na tunatarajia kupata upinzani mkubwa.
Kuhusu maandalizi kocha, Barker amesema wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri jana wamefanya mazoezi na leo watafanya ya mwisho tayari kwa mchezo wa kesho.
"Maandalizi ya mchezo yamekamilika, na leo tutafanya mazoezi ya mwisho kujiweka sawa. Tunafahamu utakuwa mchezo mgumu na tunawaheshimu TRA lakini tumejipanga kuhakikisha tunapata ushindi."
"Hatukufurahishwa na matokeo tuliyopata kwenye mechi iliyopita dhidi ya Pamba, lakini tupo nyumbani sasa tunataka kuonyesha uwezo mkubwa na kupata ushindi ili kuwafurahisha mashabiki wetu," amesema Barker.
Akizungumza kwa niaba ya wachezaji mlinzi wa kushoto, Nickson Kibabage amesema pamoja na ugumu ambao tunategemea kukutana nao lakini tumejipanga kikamilifu kupata ushindi nyumbani.
"Kwa upande wetu kama wachezaji kila mmoja yupo tayari kuhakikisha anapambana mpaka mwisho kuisaidia timu kupata ushindi," amesema Kibabage.