Simba Sports Club
News

Kauli ya Barker kuelekea mchezo dhidi ya Stade Malien

13 Feb 2026

Barker amesema malengo yetu katika mchezo wa kesho ni kuonyesha kiwango safi kwa ajili ya kupata ushindi pamoja na kuwafurahisha mashabiki wetu.

Barker ameongeza kuwa anafurahishwa na maendeleo ya wachezaji mmoja mmoja hasa wageni tuliowasajili mwezi Januari kwakuwa wanamuonyesha mwanga huku akiwaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanjani kuwapa sapoti.

"Malengo yetu ni kuhakikisha tunashinda mchezo wa kesho pamoja na kuonyesha soka safi, tutautumia pia mchezo kuimarisha kikosi chetu ambacho maendeleo yake ni mazuri," amesema Barker.

Advertisement

Kwa upande wake mshambuliaji, Seleman Mwalimu amesema tumekuwa na muendelezo mzuri katika mechi zetu za ligi zilizopita na tunataka kuendeleza kesho ili kurejesha imani na matumaini kwa mashabiki.

"Tunahitaji kushinda mchezo wa kesho ili kurejesha imani na matumaini kwa mashabiki wetu kuelekea katika michuano ya Ligi Kuu pamoja na CRDB Federation Cup," amesema Mwalimu.

Back to homepage
Share this story