Chama alijiunga nasi kwa mara ya kwanza mwaka 2018 akitokea Lusaka Dynamos ya Zambia ambapo alidumu kwa miaka minne.
Chama alirejea tena mwaka 2022 akitokea RS Berkane ya Morocco ambapo alidumu kwa miaka miwili na sasa amerudi akitokea Singida Black Stars.
Chama ni mmoja ya wachezaji wenye kipaji na uzoefu mkubwa na kipenzi cha Wanasimba.
Advertisement
Kurejea kwa Chama kutaongeza ubunifu katika idara ya kiungo cha ushambuliaji kutokana na uwezo mkubwa alionao.
Chama ni miongoni mwa wachezaji 22 watakaosafiri kesho kuelekea nchini Tunisia kwa ajili ya mchezo wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya ES Tunis utakaopigwa Jumamosi.