Yakoub (23) ndiye mlinda mlango namba moja wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kwa sasa na mechi zote ameonyesha kiwango safi.
Katika michuano iliyopita ya CHAN amecheza mechi zote za Stars huku akiisaidia kufika hatua ya robo fainali.
Yakoub anakuja kusaidiana na walinda milango wengine Moussa Camara na Hussein Abel kulifanya lango letu kuwa imara zaidi.
Advertisement
Uongozi wa klabu ya Simba na benchi la ufundi lina matumaini makubwa ya Yakoub na atakuwa msaada mkubwa kwa timu katika michuano ya ndani na Kimataifa.
Kabla ya kujiunga na Maafande wa JKT Tanzania, Yakoub alikuwa akicheza katika klabu ya JKU inayoshiriki Ligi Kuu ya Zanzibar.