Nangu (23) ni miongoni mwa wachezaji vijana wenye vipaji vikubwa ambaye tuna matumaini nae makubwa na atakuwa msaada kwa kikosi.
Nangu alikuwepo kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' iliyoshiriki michuano ya CHAN na kuishia robo fainali.
Advertisement
Nangu ambaye anaweza pia kutumika kama mlinzi wa kushoto anaungana na walinzi wengine wa kati kama Abdulazak Hamza, Karabou Chamou na Rustine De Reuck.
Nangu ana uzoefu mkubwa wa ligi Kuu ya Tanzania maana kabla ya kujiunga na JKT Tanzania alikuwa akikipiga katika klabu ya TMA Stars.