Gomez (20) ni mchezaji kijana mwenye uwezo mkubwa wa kutumia nafasi zinazopatikana na pia kufunga kwa namna zote miguu yote miwili na kichwa pia.
Kabla ya kujiunga na Waydad kwenye dirisha dogo la usajili lililopita alikuwa akikitumikia kikosi cha Fountain Gate FC huku akifunga mabao sita kwenye Ligi Kuu ya NBC.
Gomez anaijua vizuri Ligi Kuu za Tanzania kutokana nakuwahi kuzichezea pia timu za KVZ ya Zanzibar kabla ya kujiunga na Singida Black Stars huku pia akiwa na uzoefu wa michuano ya Kimataifa na hilo ni moja ya kitu kilichotuvutia.
Gomez alikuwepo kwenye kikosi cha Wydad kilichoshiriki michuano ya Kombe la Dunia la Klabu lililofanyika nchini Marekani, Juni mwaka huu.
Gomez tayari yupo jijini Dar es Salaam anasubiri kikosi kirejee leo kutoka Misri na kujiunga nacho moja kwa moja kujiandaa na msimu mpya wa mashindano 2025/2026.