Zanga (21) raia wa Cameroon ni miongoni mwa viungo bora wa ukabaji lakini pia ana uwezo mkubwa wa kuanzisha mashambulizi kupitia mipira mirefu.
Zanga ni nyota ambaye tunategemea atakuwa muhimili mkubwa wa kikosi chetu hasa pale timu itakapokuwa inashambuliwa pamoja na kuanzisha mashambulizi.
Advertisement
Mbali na kucheza kama kiungo mkabaji Zanga pia anamudu kucheza kama beki wa kushoto na beki wa kati.