Nandede (22) anaweza kumudu kucheza nafasi zaidi ya nne uwanjani na hicho ni moja ya kigezo kilichotuvutia kuhitaji saini yake.
Nandede raia wa Uganda anaweza kucheza kwa ufanisi mkubwa nafasi za winga wa kulia, kushoto, namba tisa na wakati mwingine mlinzi wa kulia.
Advertisement
Moja ya vigezo tulivyozingatia kwenye usajili wetu msimu huu ni kusajili mchezaji mwenye uwezo wa kucheza nafasi mbalimbali uwanjani ili kumpa nafasi kocha ya kupanga timu kulingana na mpinzani.