Simba Sports Club
News

Karibu Simba Queens 'Kiraka' Elizabeth Nashon

22 Sep 2025

Elizabeth (23) ni mchezaji raia wa Tanzania ambaye ana uwezo wa kucheza namba nyingi uwanjani kwa ufanisi mkubwa na hii ndio maana halisi ya mchezaji kiraka.

Elizabeth anaweza kumudu kucheza kama kiungo mkabaji namba sita, winga ya kulia, namba nane, nyuma ya mshambuliaji kama namba 10, winga ya kushoto na mlinzi wa kulia.

Advertisement

Kulingana na kipaji chake alichojaaliwa na Mwenyezi Mungu pamoja na umri wake, Elizabeth atakuwa msaada mkubwa kwa Simba Queens pamoja na timu ya Taifa ya Tanzania 'Twiga Stars'.

Back to homepage
Share this story