Heutchou (19) amejiunga na Simba Queens katika kipindi hiki cha dirisha dogo akitokea Eclair Football ya nchini kwao Cameroon.
Heutchou ni mshambuliaji kijana mwenye kipaji ambaye ana uwezo mkubwa wa kufunga na kutengeneza nafasi kwa wengine kutokana na kasi aliyonayo.
Advertisement
Msimu wa 2024/2025 alikuwa mchezaji bora chipukizi wa Ligi Kuu nchini Cameroon baada ya kufunga mabao 20.
Heutchou tayari amejiunga na kikosi na anatarajiwa kuwepo katika mchezo dhidi ya Bilo Queens wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Wanawake (WPL) utakaopigwa Aprili 3 katika Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.