Simba Sports Club
News

Karibu Simba Libasse Gueye

17 Jan 2026

Gueye (22) raia wa Senegal anaweza kucheza kama winga wa kulia pamoja na kiungo mshambuliaji yaani namba kumi.

Gueye ni mchezaji wa timu ya Taifa ya Senegal chini ya umri wa miaka 23 na amecheza mechi sita za timu ya wakubwa ya Senegal.

Alikuwepo kwenye kikosi cha Senegal kilichoshiriki michuano ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) iliyofanyika mwaka jana katika nchi za Tanzania, Kenya na Uganda.

Advertisement

Msimu wa 2022/23 Gueye alichaguliwa mchezaji bora chipukizi wa Ligi Kuu Senegal.

Gueye ni mchezaji kijana mwenye kasi na tunategemea atakuwa na mchango mkubwa kwenye safu ya ushambuliaji katika mechi za ndani pamoja na Kimataifa.

Back to homepage
Share this story