Toure (28) Raia wa Ivory Coast ni mchezaji mwenye uzoefu mkubwa wa soka la Afrika kutokana na kushiriki michuano hiyo akiwa na timu tofauti.
Toure ameshiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika akiwa na ASEC Mimosas ya Ivory Coast, Kombe la Shirikisho Afrika akiwa na timu za Marumo Galants na Stellenbosch za Afrika Kusini.
Toure ambaye pia anaweza kucheza kama kiungo wa Ulinzi ni mchezaji mrefu mwenye umbo kubwa na pia ni bora katika mipira ya juu.
Advertisement
Usajili wa Toure ni pendekezo la kocha mkuu, Steve Barker ambaye amewahi kufanya nae kazi akiwa katika klabu ya Stellenbosch.
Tunategemea Toure atakuwa msaada mkubwa kwenye kikosi chetu.