Simba Sports Club
News

Karibu Simba Inno Jospin Loemba

28 Jan 2026

Loemba (22) raia wa Congo Brazzaville ni mchezaji mbunifu mwenye uwezo mkubwa wa kucheza nafasi tofauti uwanjani kwa ufanisi mkubwa Loemba anafurahi zaidi kucheza nyuma ya mshambuliaji yaani namba 10.

Usajili wa Loemba umefanikishwa na Mzabuni wa jezi Jayrutty Investment EA Ltd, ikiwa ni moja ya ahadi iliyotoa ya kusajili mchezaji bora ambaye atapendekezwa na benchi la ufundi pamoja na uongozi.

Ahadi hiyo ilitolewa Aprili 16, 2025 na Mkurugenzi wa Jayrutty, Joseph Rwegasira baada ya kusaini mkataba wa kutengeneza na kusambaza jezi na leo ametimiza ahadi yake.

Advertisement

Uongozi wa klabu pamoja na benchi la ufundi una matumaini makubwa na Loemba na matarajio yetu atakuwa na mchango mkubwa ndani ya kikosi.

Loemba anakuwa mchezaji wa sita kujasjiliwa ndani ya kikosi chetu katika dirisha hili la usajili baada ya Libasse Gueye, Nickson Kibabage, Clatous Chama, Ismail Toure na Djibrilla Kassali.

Back to homepage
Share this story