Oura (27) raia wa Ivory Coast ana uwezo wakucheza nafasi mbalimbali katika eneo la kiungo na ushambuliaji na hicho ni moja ya kitu kilichotuvutia kuhitaji huduma yake.
Oura ana uzoefu wa soka la Afrika amewahi kuzitumikia timu za ASEC Mimosas ya nchini kwao pamoja na Stellenbosch ya Afrika Kusini.
Advertisement
Akiwa na kikosi cha ASEC amefanikiwa kutwaa mataji matatu ya Ligi Kuu nchini Ivory Coast.
Huu ni usajili wa sita tuliyofanya kwenye dirisha hili dogo baada ya Libasse Gueye, Nickson Kibabage, Clatous Chama, Ismail Toure na Mamadou Djibrilla.