Simba Sports Club
News

Karibu Nyumbani Jentrix Shikangwa

11 Jan 2024

Jentrix raia wa Kenya amerejea Simba Queens baada ya kupita miezi sita tu baada ya kujiunga na Jingtan Julai mwaka jana.

Wakati anaondoka kuelekea China, Jentrix alikuwa mfungaji bora Ligi Kuu ya Wanawake huku akifunga mabao 25.

Advertisement

Jentrix alijiunga nasi katika dirisha dogo la usajili Disemba mwaka 2022 na akacheza nusu msimu kabla ya kupata dili la China na sasa amerejea nyumbani.

Tunaamini uwezo wa Jentrix na kwa kusaidiana na wenzake aliowakuta tunaamini tutafanya vizuri na kurejesha mataji tuliyopoteza msimu uliopita.

Back to homepage
Share this story