Kapombe aligongana kichwani na mshambuliaji wa Biashara Atuple Green katika harakati za kuwania mpira na kusababisha kufanyiwa mabadiliko dakika ya 28.
Kabla ya kutolewa Kapombe alikuwa amechangia upatikanaji wa mabao mawili (Assist) yaliyofungwa na Pape Sakho na Mzamiru Yassin.
Kapombe alipatiwa matibabu ya huduma ya kwanza kutoka kwa wauguzi wa Uwanja wa Benjamin Mkapa na kisha kupelekwa hospitali kwa vipimo zaidi.
Advertisement
Baada ya vipimo hivyo imebainika kuwa hajapata madhara yeyote ya kichwa na kwamba yuko salama tofauti na ilivyotarajiwa.
Licha ya kutopata madhara lakini madaktari wamempa mapumziko ya siku tano kutokana na mgongano huo ili kumkinga na kumfanya awe salama zaidi.