Kapombe amesema maandalizi ya mchezo yanaendelea vizuri na wachezaji wote 21 waliosafiri kuja nchini Mali wapo kwenye hali nzuri na wapo tayari kwa mchezo.
Kapombe amekiri kuwa tunategemea kupata upinzani mkubwa kutoka kwa Malien hasa kutokana wakiwa wapo nyumbani lakini tupo tayari kuwakabili.
Advertisement
Aidha Kapombe ameongeza kuwa pamoja ugumu ambao tunategemea kukutana nao lakini tutaingia kwenye mchezo wa Jumapili kwa lengo la kutafuta matokeo chanya.
"Maandalizi yanaendelea vizuri, wachezaji wote tuliokuja huku Mali tupo tayari kwa mchezo na tunafahamu utakuwa mgumu lakini tumejipanga na tupo tayari," amesema Kapombe.