Baada ya mchezo wa kesho utakaopigwa Uwanja wa Ushirika Moshi tutaanza maandalizi ya mchezo huo wa robo fainali hivyo Kapombe ameweka wazi kuwa tukishinda tutakuwa katika nafasi nzuri.
Kapombe ameongeza kuwa mchezo wa kesho utakuwa mgumu kutokana na ubora wa wapinzani na ugumu wa ratiba kwetu lakini tumejipanga vizuri kuhakikisha tunashinda.
Advertisement
"Kwa sasa kila mchezo kwetu ni fainali, tunahitaji kushinda ili kupunguza tofauti ya alama tulizoachwa na wanaoongoza.
"Tunahitaji kushinda kesho ili kuongeza morali kuelekea mchezo wetu wa Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Orlando Pirates utakaofanyika wikiendi ijayo," amesema Kapombe.