Simba Sports Club
News

Kapombe mbioni kusaini mkataba mpya

14 May 2023

Kapombe amethibitisha hilo kwenye mahojiano aliyofanya na Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu, Ahmed Ally kupitia Simba App.

Kapombe amesema mkataba wake unafikia ukingoni mwishoni mwa msimu huu na tayari wasimamizi wake wameanza mazungumzo na viongozi kwa ajili ya mkataba mpya.

"Kwa sasa sifikirii kwenda klabu yoyote zaidi ya kubaki Simba, mkataba wangu unaelekea ukingoni lakini wawakilishi wangu wanaendelea na mazungumzo na viongozi naamini tutafikia makubaliano mazuri," amesema Kapombe.

Kapombe ni miongoni mwa wachezaji waandamizi ndani ya klabu yetu akiwa amedumu tangu mwaka 2011 ingawa aliwahi kuondoka kabla ya kurejea tena.

Advertisement

Mlinzi huyo wa kulia amekuwa msaada mkubwa kwenye kikosi chetu akishiriki kuchukua ubingwa mara nne mfululizo na kutinga robo fainali tatu za ligi ya Mabingwa Afrika na moja ya Kombe la Shirikisho.

Kapombe anategemewa kuwa mchezaji wa pili kuongeza mkataba mpya baada ya mlinzi wa kati Henock Inonga kufanya hivyo mwezi Desemba mwaka jana.

Kwa sasa uongozi upo kwenye mazungumzo ya kuwaongezea mikataba wachezaji ambao wapo kwenye mipango ya timu kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi 2023/24.

Back to homepage
Share this story