Kapombe alishindwa kuendelea na mchezo baada ya kuumia goti katika harakati za kugombea mpira na mchezaji wa Raja na kutolewa kwa msaada wa machela.
Matibabu ya awali yaliyofanyika uwanjani yalionesha kuwa goti lake halikupata madhara makubwa kwani baada ya mchezo aliweza kutembea mwenyewe bila usaidizi.
Daktari wa timu, Edwin Kagabo anasema baada ya timu kuwasili leo jijini Dar es Salaam, Kapombe atafanyiwa vipimo ili kubaini athari ya jeraha lake.
"Kwa uchunguzi wa awali haionekani kama ni jereha kubwa na kwamba anaweza kupewa mapumziko ya siku chache kabla ya kurudi tena uwanjani," amesema Dr. Edwin.
Kwa upande wa Kibu nae alipata jeraha la goti hivyo nae baada ya timu kuwasili atafanyiwa vipimo kujua maendeleo yake.
Mchezaji mwingine ambae anatakiwa kufanyiwa vipimo ni Peter Banda ambae aliumia bega kwenye majukumu ya timu yake ya taifa ya Malawi 'The Flames'.
Baada ya kuumia Banda alishindwa kujiunga na timu Morocco hivyo ilimbidi kurejea moja kwa moja jijini Dar es Salam kuendelea na vipimo.
"Nimepokea taarifa ya majeraha ya Banda kutoka timu ya taifa ya Malawi lakini wao pia wanahitaji kujiridhisha kwa vipimo ili kuangalia kwanini bega lilimekuwa likimsumbua mara kwa mara," amesema Dk. Edwin.