Simba Sports Club
News

Kapombe azungumzia maendeleo ya kambi nchini Misri

13 Jul 2024

Kapombe amesema Kocha Mkuu Fadlu Davids amekuwa akiwafundisha vitu vipya huku akisisitiza katika mazoezi ya stamina ili wawe imara.

Kapombe ameongeza kuwa ikiwa leo ni siku ya tano tangu tuanze kambi ya maandalizi hapa Misri, wachezaji wanajitahidi kufuatia maelekezo wanayopewa.

Advertisement

"Kambi inaendelea vizuri hapa Misri, tunazidi kupokea mafunzo kutoka kwa walimu wetu. Kocha anasisitiza tuwe haraka sana tunaposhambulia na kutumia kwa ufasaha nafasi."

"Leo ni siku ya tano tangu tuanze kambi ya maandalizi naamini hadi tukimaliza tutakuwa imara na tayari kwa mashindano," amesema Kapombe.

Back to homepage
Share this story