Simba Sports Club
News

Kapombe awaita mashabiki kwa Mkapa Kesho

20 Feb 2023

Kapombe amesema uwepo wa mashabiki ni muhimu na wana mchango mkubwa katika mchezo hivyo ni jambo jema kama watajitokeza kwa wingi uwanjani kuwapa sapoti ili tupate alama tatu.

"Tunawahitaji sana mashabiki wetu kuja kwa wingi uwanjani kesho, uwepo wao ni muhimu na wanatupa nguvu ya kupambana kupata alama tatu," amesema Kapombe.

Akizungumzia hali ya kikosi Kapombe amesema:

Advertisement

"Walimu wameendelea kutupa maandalizi mazuri ya mwisho, tumefanya mazoezi tumehakikisha tunafuata maelekezo yote tuliyopewa.

"Tunajua utakuwa mchezo mgumu, tunaiheshimu Azam lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda na kupata alama tatu muhimu," amesema Kapombe.

Back to homepage
Share this story