Mlinzi wa kulia Shomari Kapombe, amerejea mazoezini pamoja na wachezaji wenzake baada ya kupona majeraha yaliyokuwa yanamsumbua.
Kapombe alipata majeraha ya mguu katika mchezo wa ufunguzi wa ligi dhidi ya Biashara United uliopigwa Uwanja wa Karume mkoani Mara Septemba 28, ambapo alishindwa kuendelea na mechi.
Advertisement
Kutokana na majeruhi hayo Kapombe aliukosa mchezo wa pili wa ligi dhidi ya Dodoma Jiji pamoja na mechi mbili zaTimu ya Taifa ya Tanzania za kufuzu Fainali ya Kombe la Dunia dhidi ya Benin.
Kapombe anaungana na Sadio Kanoute ambaye alipata maumivu ya bega kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii na kukosa mechi mbili za ligi ambaye naye amerejea uwanjani wiki iliyopita baada ya kupona.