Simba Sports Club
News

Kapombe aibeba Stars dakika za jiioooni!!

6 Aug 2025

Kapombe alifunga bao hilo dakika ya 88 kwa shuti kali akiwa ndani ya sita baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Idd Suleiman 'Nado'.

Katika mchezo huo Mauritania walikuwa bora zaidi kipindi cha kwanza huku wakifanya mashambulizi zaidi lakini tulikuwa imara kuhakikisha tunawadhibiti.

Kipindi cha pili tulirudi kwa kasi na kufanya mashambulizi mengi huku Mauritania wakicheza kwa kuzuia na kushambulia kwa kushtukiza.

Advertisement

Ushindi huu unaifanya Tanzania kuwa vinara wa kundi B na kufikisha pointi sita, tukifunga mabao matatu huku tukiwa hatujaruhusu bao lolote.

X1: Yakoub, Kapombe, Zimbwe Jr, Bacca, Job, Kagoma (Pipino 45' Shekhan 75') Nado (Msindo 90'), Mudathir, Mzize, Feisal, Sopu (Saadun 45')

Waliionyeshwa kadi: Kagoma, Mzize

Back to homepage
Share this story