Simba Sports Club
News

Kapombe aelezea maana ya staili yake ya kushangalia

20 Nov 2022

Kapombe alifunga bao hilo dakika ya 36 akimalizia pasi ya Clatous Chama ambapo alikaa kitako na kuinua mikono juu kuashiria kumshukuru Mungu.

Kapombe ameendelea kusema baada ya kusumbuliwa na majeraha tangu kuanza kwa msimu ameona ni jambo jema kumshukuru Mungu kwa kumuwezesha kufunga bao la kwanza baada ya kupona majeraha.

"Maana ya staili yangu ya ushangiliaji ni kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunisaidia kuwa na afya njema. Nimeanza msimu kwa kusumbuliwa na majerah lakini namshukuru Mungu sasa nipo fiti," amesema Kapombe.

Advertisement

Kabla ya kurejea katika mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar uliopigwa Oktoba 30 mara ya mwisho Kapombe kucheza ilikuwa Septemba 14 kwenye mechi dhidi ya Tanzania Prisons iliyopigwa Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Mechi ya jana ilikuwa ya nne mfululizo kwa Kapombe kucheza tena dakika zote 90 baada ya kushuka dimbani dhidi ya Mtibwa, Singida Big Stars, Namungo na Ihefu FC.

Back to homepage
Share this story