Kapombe amesema kila siku baada ya mazoezi ya kawaida kumekuwa na muda kupiga penati na hilo ndilo lilimpa ujasiri wa kwenda kubeba jukumu hilo.
Tangu kuanza kwa msimu tumekuwa na wimbi kubwa la kukosa penati katika kikosi chetu hivyo Kapombe anasema hayakuwa maamuzi rahisi kwenda kuchukua jukumu hilo.
"Tunafanya mazoezi ya kupiga penati kila siku lakini jana tulihitaji kushinda ile penati kwa sababu dakika zilikuwa zimekwenda sana na tulihitaji ushindi nyumbani.
"Wakati nakwenda kupiga nilikuwa namuomba Mungu anisaidie nipate, pia nilikuwa naifikiria timu, familia yangu pamoja na mashabiki ambao walikuwa wanahitaji furaha kwa wakati ule na namshukuru Mungu nilifanikiwa," amesema Kapombe.
Kapombe amewaomba mashabiki waendelee kujitokeza uwanjani kuisapoti timu kwa kuwa nyakati za furaha zimeanza kurejea taratibu.