Simba Sports Club
News

Kanoute, Sakho, Mzamiru fiti asilimia 100

8 Nov 2021

Wachezaji wetu watatu waliokuwa majeruhi viungo Sadio Kanoute, Pape Ousmane Sakho na Mzamiru Yassin wamepona majeraha yao na wamerudi uwanjani wakiwa fiti asilimia 100.

Kanoute na Sakho wameanza mazoezi pamoja na wenzao leo wakati Mzamiru amejiunga na kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kinachojiandaa na mechi ya kufuzu fainali ya Kombe la Dunia dhidi ya DR Congo.

Kikosi kimerejea mazoezini leo baada ya mapumziko ya siku nne ambapo asubuhi walikwenda gym na jioni wakifanya uwanjani.

Advertisement

Kiungo Taddeo Lwanga yeye bado anauguza jeraha na amepewa mapumziko ya wiki mbili kabla ya kurejea uwanjani.

Taddeo raia wa Uganda anatarajiwa kurejea kabla ya mchezo wetu wa ligi dhidi ya Ruvu Shooting utakaopigwa Uwanja wa CCM Kirumba, Novemba 19.

Aidha, mshambuliaji Chris Mugalu ataendelea kukosekana sababu ya jeraha linalomsumbua kutokupona vizuri hivyo amepewa muda zaidi ili awe fiti asilimia 100.

Back to homepage
Share this story