Kiungo Sadio Kanoute na mlinzi Joash Onyango hawatakuwa sehemu ya kikosi kitakachosafiri kwa ajili ya mechi mbili za kwanza za ligi dhidi ya Biashara United na Dodoma Jiji kutokana na kuwa majeruhi.
Kanoute amepata maumivu ya bega baada ya kuumizwa na mchezaji Yanick Bangala katika mchezo wa jana wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga na kushindwa kuendelea na mechi huku Onyango nae akiumia kichwani katika jitihada za kutafuta bao la kusawazisha ambapo pia alishindwa kuendelea na mchezo.
Nyota hao wapo chini ya uangalizi wa daktari kufuatilia hali zao na tunatarajia watajiunga na kikosi baada ya kurejea jijini Dar es Salaam.
Kikosi kitaondoka leo saa 12 jioni kuelekea jijini Mwanza na kesho asubuhi kitaenda mkoani Mara tayari kwa mechi ya kwanza ya ligi dhidi ya Biashara itakayochezwa Jumanne Uwanja wa Karume saa 10 jioni.