Kanoute aliumizwa mguuni na kiungo wa Yanga Khalid Aucho na kushindwa kuendelea na mchezo na kudhaniwa amepata madhara makubwa lakini baada ya vipimo vya madaktari ameonekana hana tatizo.
Kanoute atakosa michezo miwili ya ligi dhidi ya Ruvu Shooting na Azam na wa Robo Fainali ya Azam Sports Federation Cup tutakaocheza na Pamba.
Advertisement
Kiungo huyo ambaye hana mambo mengi uwanjani zaidi ya kukaba anatarajiwa kurudi uwanjani Mei 22, katika mchezo wa Ligi dhidi ya Geita Gold utakaopigwa Uwanja wa CCM Kirumba.