Simba Sports Club
News

Kanoute apewa mapumziko ya siku mbili

5 Feb 2023

Kanoute alitolewa dakika ya 83 kwa machela baada ya kupata maumivu hayo hali iliyozua hofu kwa mashabiki na wapenzi lakini nyota huyo kutoka Mali hakupata madhara makubwa.

Daktari wa timu, Edwin Kagabo ameiambia Simba App kuwa Kanoute aliangukia nyonga hivyo kupata maumivu yaliyomfanya ashindwe kuendelea na mchezo lakini haikuwa tatizo kubwa.

Baada ya vipimo imebainika hakupata madhara makubwa hivyo amepewa mapumziko ya siku mbili ambapo kesho Jumatatu atarejea mazoezini kuendelea na program ya mazoezi.

Advertisement

Akizungumzia hali ya majeruhi kwa ujumla Dk. Edwin amesema kwa sasa hakuna mchezaji ambae ni majeruhi na wote waliokua wanaosumbuliwa na maradhi mbalimbali wameshapona na wamerejea kikosini.

"Kanoute alipata maumivu ya nyonga, amefanyiwa vipimo na ameonekana hajapata madhara makubwa amepewa mapumziko ya siku mbili na kesho atarejea mazoezini na wenzake," amesema Dk. Kagabo.

Back to homepage
Share this story