Kampeni ya leo imeanzia Makao Makuu ya klabu na kuzunguka mitaa mbalimbali ya Kariakoo, ikaenda Karume na kumalizia soko la Ilala.
Kampeni tuliizindua jana Tegeta katika Tawi la Wazo Hill ambapo tumeendelea na zoezi la kuuza tiketi za mchezo pamoja na jezi.
Advertisement
Muamko wa Wanasimba ni mkubwa wamejitokeza kwa wingi kununua tiketi kwa ajili ya kuipa sapoti timu kwenye mchezo huo mkubwa unaosubiriwa kwa hamu.
Lengo letu ni kuhakikisha tunapambana kwa kila hali ili tuweze kupata ushindi katika Uwanja wa nyumbani.